Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Ramadhan Kingai
DCI Kingai ameyasema hayo jijini Mwanza wakati akizungumza na maafisa waandamizi wa jeshi la polisi jijini Mwanza katika kikao maalum cha kuwakumbusha majukumu yao kwa lengo la kuendelea kupunguza vitendo vya uhalifu
"Watu wanohitaji dhamana kusiwe na kona nyingi mpaka tunapokea kauli kwamba kuingia polisi ni bure kutoka na hela, tusikubali kutoa nafasi ama fursa ya maneno kama hayo kutawala tusimamie haki tuwajibike sawasawa" amesema DCI Kingai
Aidha katika hatua nyingine DCI Kingai amesema ulinzi shirikishi unasaidia kupunguza matukio ya uhalifu hivyo ni vyema askari wakashiriki vizuri katika ulinzi shirikishi ili kuzuia makosa hayo yasiendelee kutokea
"Hatuwezi kufika kila sehemu kama ambavyo ilikuwa nia ya uanzishwaji wa ulinzi shirikishi kwa sasababu polisi ni wachache na maeneo ni makubwa hatuna vituo vya polisi vilivyosambaa kila sehemu tukawa na nguvu ya uhakikka ulinzi shirikishi ndiyo utatusaidia kupunguza matukio ya uhalifu," ameongeza.