
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa rai hiyo wakati akihutubia viongozi mbalimbali (hawapo pichani)kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Ubunifu wa Afya Duniani (World Innovation Summit for Health) uliofanyika hii leo Doha nchini Qatar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa rai hiyo wakati akihutubia viongozi mbalimbali kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Ubunifu wa Afya Duniani (World Innovation Summit for Health) uliofanyika hii leo Doha nchini Qatar.
Rais samia amesema mkutano huo umelenga kuhamasisha mipango bora ya afya kidunia na kwamba Tanzania imepanga kuongeza ushirikiano katika kufikia utekelezaji wa mpango wa umoja wa mataifa wa mwaka 2030 na ule wa Tanzania kufikia mwaka 2025.
Hata hivyo amesisitiza kuwa ukuaji wa miji utandawazi,umeifanya dunia kuwa na changamoto katika kupanga sera rafiki kwa afya ikiwemo udhibiti wa magonjwa hatari kama ilivyokuwa kwa covid 19 ugonjwa ambao ulikuja na kuacha mafunzo kwa mataifa duniani huku yale yanayoendelea yakisubiri chanjo kutoka mataifa ya magharibi.
Mkutano huo wa Ubunifu wa Afya Duniani (World Innovation Summit for Health) umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kujadili namna ambavyo mataifa yanaweza kutumia bunifu katika kuimarisha afya za watu wao.