
Picha ya jangwa
Hayo yamebainishwa jijini Mwanza na Meneja wa wakala wa misitu TFS kanda ya ziwa, Bakari Salim baada ya zoezi la upandaji miti lililoambatana na utoaji wa taulo za kike katika shule ya sekondari ya wasichana lugeye iliyopo wilayani Magu shughuli iliyoratibiwa na shirikisho la walimu Mkoa wa Mwanza na kusema kuwa ili kuinusuru Mikoa hiyo ipo haja ya kupanda miti mingi.
kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima ameahidi kufanya zoezi la upandaji miti kuwa endelevu ili kukabiliana na changamoto hiyo ya ukame katika maeneo mbalimbali Mkoani humo.