
Mapigano hayo yanasemekana kuwa mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miezi ya hivi karibuni.
Ghasia hizo zilizuka wiki iliyopita kufuatia mzozo wa ardhi kati ya watu wa Jamii ya Hausa na makabila hasimu, ambapo zaidi ya watu 12 waliuawa.
Amri ya kutotoka nje usiku ilitangazwa ili kudhibiti ghasia hizo.
Umoja wa Mataifa usema kwamba "umeshtushwa na kuongezeka kwa ghasia huko Lagawa na kuzuka tena kwa mzozo katika eneo la Blue Nile.
Umoja huo umesema kwamba amani endelevu haitawezekana bila serikali ya kuaminika kikamilifu ambayo inatoa kipaumbele kwa mahitaji ya jamii za wenyeji ikiwa ni pamoja na usalama na kushughulikia chanzo cha migogoro.
Sudan imekuwa ikikabiliana na machafuko ya kisiasa na ghasia tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka jana.