
Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wakuu wa Vikosi wakiwa hifadhi ya taifa ya Mikumi
Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wakuu wa Vikosi wamewaonya baadhi ya
watu wanaofanya vitendo vya ujagili na kuharibu baadhi ya vivutio mbalimbali vya
taifa ambavyo ni urithi wa vizazi vijavyo.
Akiwaongoza kutembelea hifadhi ya taifa ya Mikumi, kamishna wa Utawala na
Menejimenti ya Rasilimali Watu CP Benedict Wakulyamba amesema kuwa,
kufuatia uzinduzi wa filamu ya Royal Tour imesaidia kufunguka kwa utalii nchini
ambapo watu mbalimbali wamekuwa wakitembelea hifadhi pamoja na vivutio
vilivyopo.
Aidha, kamishna Wakulyamba, amewataka wananchi na Watanzania kwa ujumla
kuendelea kulinda rasilimalia za taifa pamoja na kutembelea na kufanya utalii wa
ndani.