Ijumaa , 18th Nov , 2022

Mkutano wa kilele wa wiki mbili wa COP27 nchini Misri unaingia siku yake ya mwisho hii leo huku wajumbe wakiendelea kupambania baadhi  ya suluhu walizokubaliana.

Moja na suluhu hizo ni  pamoja na kiwango gani cha nchi zicnazochangia uchafuzi wa hali ya hewa zinapaswa kukabiliana na kutoa malengo ya hali ya hewa, na ufadhili kwa nchi zinazoendelea zilizoathiriwa zaidi na athari za hali ya hewa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema mambo ya kulaumiana yamepelekea kichocheo cha uharibifu wa pande zote.

Amesema uaminifu kati ya nchi tajiri na maskini umevunjika, na akawataka wakubaliane juu ya kile alichokiita makubaliano kabambe na ya kuaminika.
Kushindwa kupata suluhu ya makubaliano hii leo katika  kutatua masuala bora kunaweza kpelekea wapatanishi kuendelea na kazi ya upatanishi mpaka mwishoni mwa wiki hii.