
Chatu huyo alikua na ukubwa wa takriban mara tatu ya umbo la kijana huyo.
Kwa mujibu wa baba yake mzazi Kijana Beau Blake alikuwa akifurahia kuogelea nyumbani kwao wakati chatu huyo mwenye urefu wa mita 3 sawa na futi 10 alipomvamia.
Lakini Beau yuko katika hali nzuri na kwamba anaendelea vyema ingawa ana majeraha madogo tu.
Tukio hilo limeendelea kuzungumziwa katika eneo analoishi kijana huyo.