
Taarifa ya TAMISEMI imeeleza kuwa Idadi ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza Januari, 2023 imeongezeka kwa wanafunzi 166, 139 sawa na ongezeko la asilimia 18.30 ikilinganishwa na Wanafunzi 907, 802 waliopata alama ya kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka, 2022
Kati waliofaulu na kupangiwa kujiunga na kidato cha kwanza wamo wanafunzi wenye mahitaji maalum 2, 775 sawa na asilimia 0.26 ambao kati yao wavulana ni 1, 491 na wasichana 1, 284