Jumatatu , 16th Mar , 2015

Unapozungumzia vijana wanaofanya poa kwa sasa katika gemu la Afrika Mashariki huwezi acha kumtaja Mt number one, jamaa kutoka Burundi lakini makazi yake kwa sasa ni USA.

Mt Number one naye ni msani wa kizazi kipya na hadi sasa ameshatoa album mbili ambazo zote ziko kwenye soko la kimataifa (international market) kama iTunes and Amazon na hata ukitembelea YouTube zinapatikana.

Mt Number one alianza muziki mwaka 2012 na hadi sasa ameendelea kufanya vyema hadi kufungua studio yake.

“Lengo langu ni kufanya muziki kwa kusapoti wenzangu pia nchi yangu ya Burundi na Afrika Mashariki kwa ujumla .Ingawa niko Marekani kwa sasa ila nimeshajenga studio yangu huko Burundi na pia nataka muziki wetu wa Afrika Mashariki ujulikane kila kona duniani”. Amesema Mt Number one

Ukisikiliza muziki wake na ukiangalia studio ambayo tayari ameiandaa utaelewa vizuri lengo la Mt Number one la kuufikisha mbali muziki wa kizazi kipya. Bofya link hii kutazama moja ya kazi yake https://www.youtube.com/watch?v=bBj1WQctVnw&app=desktop

https://www.youtube.com/watch?v=zMAyUNwHUcE&app=desktop