Ijumaa , 6th Jun , 2025

Idara ya Uhamiaji nchini imesema kuwa leo Juni 6, 2025, katika kituo cha uhamiaji cha mpaka wa Namanga mkoani Arusha, Godbless Lema alizuiliwa kutoka nchini na pasipoti yake ya kusafiria kushikiliwa na kumtaka aripoti katika ofisi ya Uhamiaji makao makuu kwa ajili ya mahojiano zaidi. 

Godbless Lema

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Idara hiyo SSI. Paul Mselle, imesema kwamba utaratibu uliotumika kumzuia Lema kutoka nchini ni wa kawaida na unatumika kwa raia yeyote pale ambapo Idara imepata taarifa zinazohitaji mhusika kuhojiwa. 

"Aidha, Idara ya Uhamiaji inatoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa za uongo zilizochapishwa na ndg. Lema kupitia mitandao ya kijamii kuwa zuio hilo linawalenga viongozi wote wa CHADEMA," imesisitiza taarifa hiyo.