Jumanne , 30th Sep , 2025

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, ametangaza kulivunja baraza lake la mawaziri kufuatia maandamano mabaya Zaidi kuripotiwa kwenye kisiwa hicho, raia wakipinga kukatika kwa umeme mara kwa mara pamoja na uhaba wa maji, watu 22 wakiripotiwa kufa tangu yalipoanza wiki iliyopita.

Katika hotuba kwa taifa hilo, rais Rajoelina alitangaza kusitisha majukumu ya waziri mkuu Wake na kuvunja serikali yake, akisema maombi ya kiti cha waziri mkuu mpya yatapokolewa ndani ya siku tatu kabla kuunda serikali mpya, Hata hivyo akisema waziri mkuu Christian Ntsay pamoja na mawaziri wengine watasalia ofisini kwa kipindi cha mpito .

Rais Rajoelina tayari alikuwa amemfuta kazi waziri wake wa kawi siku la Ijumaa, wakati huu Asilimia 36 ya raia wa Madagascar licha ya kuwa na umeme lakini umekuwa sio wa kuaminika kwa kukatika mara kwa mara.

Kampuni ya usambazaji umeme Jirama, imekuwa ikichapisha kila siku ratiba ya mgao wa umeme na siku ya Alhamisi, maandamano yalizuka katika jiji kuu la Antananarivo na kulazimu polisi kuingilia kati ambapo serikali ililazimika kutangaza amri ya kutotoka nje siku moja baadaye.