Mbunge ampongeza Rais Samia kwa kunyanyua kilimo
Mbunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameonesha kwa vitendo azma yake ya kuinyanyua sekta ya kilimo na wakulima ili izidi kutoa ajira kwa Watanzania wengi zaidi.