"Mnatufanya sisi ni wa Msumbiji"- Mbunge Katani
Mbunge wa Tandahimba Katani Ahmed Katani, amehoji kama watu wa Lindi na Mtwara ni wa Msumbiji na si Tanzania kutokana na kwamba mara nyingi wamekuwa wakiwekwa kwenye mipango ya miradi yote ya maendeleo lakini haitekelezwi ikiwemo ile ya maji, barabara na umeme.