
Mbunge wa Tandahimba Katani Ahmed Katani
Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 12, 2022, bungeni jijini Dodoma, wakati akitoa mchango wake kufuatia hoja ya hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji iliyosomwa leo na Waziri wa Wizara hiyo Jumaa Aweso.
"Tumekosea nini Taifa hili, kwenye barabara, maji tukija kwenye umeme shida, sisi watu wa Lindi na Mtwara tumekosea nini hili Taifa, au ile mipaka mnatufanya sisi watu wa Msumbiji sio wa Tanzania, leo mnapata fedha mradi wa maji wa Makonde mmeutoa," amesema Katani Ahmed Katani
Aidha mbunge huyo ameongeza kuwa "Tandahimba maji yananunuliwa mpaka Tsh 2000 kwenye bajeti hii watu ambao walishawahi kuwa na miradi ya bilioni 400 wanaongezewa fedha, Lindi na Mtwara hakuna kinachoonekana kwani sisi ni watu wa Msumbiji au Tanzania kama wengine wanaopata keki ya Taifa".