Muwe na utamaduni wa kuzungumza - Waziri Gwajima
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameiasa jamii kupitia familia zao kuweka utamaduni wa kuzungumza masuala mbalimbali yanayowahusu ili kuepukana na migogoro na uwepo wa vitendo vya ukatili katika jamii.