"Chunguzeni mishahara kwa wafanyakazi" - Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameiagiza Wizara Ujenzi pamoja na wataalam kukutana na idara ya kazi ya mkoa wa Mwanza ili kuchunguza kama kuna madai yoyote ya mishahara kwa wafanyakazi wanaojenga daraja la Kigongo Busisi maarufu kama daraja la JPM ili waweze kulipwa na ujenzi usisimame.