Wanafunzi waliorudishwa wawasilishe taarifa TCU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wanafunzi waliokuwa wanasoma katika vyuo mbalimbali nje ya nchi ambao walirudishwa nchini kufuatia kuzuka kwa janga la UVIKO19 pamoja na kuibuka kwa vita kati ya Urusi na Ukraine wawasilishe taarifa zao Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).