Benki ya Dunia kuipiga jeki Tanzania
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuahidi kuisaidia Tanzania kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na madhara ya UVIKO-19 na vita vinavyoendelea baina ya Urusi na Ukraine.