Biashara United, wainyuka Azam FC mabao 2-0
Klabu ya Biashara United imepanda kwa nafasi 2 kwenye msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara na kujiondoa kwenye mstari wa kushuka daraja baada ya kuinyuka Azam FC mabao 2-0 kwenye mchezo pekee wa Ligi uliochezwa leo, katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

