Yanga kutafuta ushindi wa kwanza Tanga, tangu 2015
Timu ya Wananchi Yanga SC inakibarua cha kuvunja mwiko wa kutopata ushindi katika uwanja wa Mkwakwani uwanja wa nyumbani wa Coastal Union ya Tanga. Mara ya mwisho Yanga kushinda Tanga dhidi ya Coastal kwenye ligi ilikuwa mwaka 2015.