Waziri atoa maagizo haya kwa Polisi wa Airport
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameagiza maofisa watano wa polisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuchukuliwa hatua za kinidhamu baada ya intelijensia yake kubaini wanajihusisha na matukio ya ukiukwaji wa maadili.