Kikosi cha Taifa Stars CHAN 2021, chatajwa
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinachojiandaa na michuano ya timu za taifa kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani barani Afrika 'CHAN', kimewekwa wazi na TFF baada ya kuchaguliwa na benchi la ufundi la timu hiyo likiongozwa na kocha mkuu Etiene Ndayiragije.