Nandy afunguka 'kukuwadiwa' wanaume
Msanii wa muziki wa bongo fleva Nandy ambae anafanya vizuri kwa sasa na wimbo wake wa 'kivuruge' amefunguka na kudai hakuna mtu yeyote atakaeweza kumuunganishia kwa wanaume wenye pesa (pedeshee) bali kama watamuitaji wataenda wenyewe kwake.

