Mzee Akilimali amchana Ngoma
Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amemtaka mshambuliaji wa timu hiyo, Mzimbabwe, Donald Ngoma, asiwayumbishe kwa chochote, na kama amepanga kuondoka kwenye timu hiyo anaweza kufanya hivyo kwani wapo watakaoziba nafasi yake.

