Walimu wa Sayansi wastaafu kurudishwa makazini
Serikali ya Tanzania imesema kuwa katika kumaliza tatizo la walimu wa sayansi nchini serikali itatoa kipaumbele cha ajira kwa walimu wa masomo hayo lakini pia wataandaa utaratibu maalumu wa kuwarejesha walimu wastaafu wa masomo ya Sayansi.

