Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Aliyosema Lissu baada ya kutolewa nje

Wednesday , 18th Oct , 2017

Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu imesema kwamba kwa mara ya kwanza ndugu yao alipotolewa nje kupata hewa na kuota jua kauli yake aliyoitoa alisema kuwa ni sawa na ukiwa mfungwa huoni jua, mawingu wala hupigwi upepo wa kawaida.

Katika mahojiano aliyofanyiwa Kaka wa Lissu,  Wakili Alute Mughwai Lissu amesema kwamba mara baada ya ndugu yake kutolewa nje na kukaa kwa takribani dakika 30 siyo yeye Lissu peke yake aliyefurahi bali ndugu wote waliokuwepo hospitalini hapo walifurahia mno hilo tukio.

Bw. Alute amesema kwamba awali Manesi walipanga kumtoa nje Jumamosi (Oktoba 14) na kwa kuwa Lissu alijua tunakwenda, aliwaeleza wasimtoe bali wasubiri ndugu zake wafike. 

"Nilikuwa mimi na ndugu wengine. Ilipofika saa 10 jioni tulimtoa na mimi ndiye nilimtoa ICU, alifurahi na sisi tulifurahi kwa hatua hiyo,” amesema Kaka huyo mkubwa wa Lissu.

Alute ameeleza kwamba baada ya Lissu kupata upepo wa nje kwa nusu saa nzima alirudishwa wodini ambako amefafanua siyo ICU tena ingawa pia kuna ulinzi na uangalizi wa karibu na si kila mtu anaweza kumwona na kuongeza kwamba hali ya ndugu yake inazidi kuimarika huku akili  zake zikiwa  timamu.”

Pamoja na hayo Alute amesema kwamba suala la kumpeleka sehemu tofauti ya matibabu ndugu yao familia ndiyo itakayoshughulika zaidi kwa ukaribu na kuongeza kwamba,  ndugu wengine wapo sehemu mbalimbali kama Kenya, Australia, Marekani, Canada ambao watabidi wajadiliane kwanza ndipo watatoa taarifa juu ya nini ya kinaendelea.

HABARI ZAIDI

Bw. Nazar Nicholas (katikati) akikabiziwa tuzo ya WSIS 2024

Tanzania yashinda Tuzo WSIS 2024, nchini Uswisi

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton