Monday , 10th Oct , 2016

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu barani Afrika yenye lengo la kukuza uhusiano na bara hilo.

Kansela wa Ujerumani akiwa na Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita wakizungumza na waandishi wa habari

Kituo chake cha kwanza kilikuwa Mali, ambapo kuna zaidi wa wanajeshi 500 wa Ujerumani, ambao wanakabiliana na wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu kwa upande wa Kaskazini mwa taifa hilo.

Katika mikutano yake na maafisa, Merkel anatarajiwa kujadili vita dhidi ya wafuasi wa itikadi kali, sambamba na hitaji kubwa umadhubuti wa kiuchumi barani Afrika kwa lengo la kukabiliana na wimbi la uhamiaji barani Ulaya.

Akitoka nchini Mali Kansela Merkel ataelekea Niger baadaye Ethiopia.