Tuesday , 26th May , 2015

Rapa Rabbit aka Kaka Sungura ameshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha baada ya tukio hatari la kuvamiwa na majambazi watatu waliokuwa na silaha ndani ya mgahawa mmoja Madaraka jijini Nairobi Kenya na kuibiwa vitu mbalimbali vya thamani.

Rabbit

Kwa mujibu wa Rabbit mwenyewe, moja ya majambazi hao ambao hawakuficha sura zao alimfuata na kukoki bastola na kumueleza kuwa angemfyatulia risasi, na kuchukua simu yake mpya, laptop pamoja na simu na saa za kila aliyekuwa eneo hilo.

Staa huyo ameweka video ya tukio hilo la kuibiwa mtandaoni na kumuomba yeyote ambaye atauziwa vitu hivyo vya wizi kumsaidia kumrejeshea data ambazo zipo ndani ya laptop hiyo kutokana na umuhimu wake kwake.