Wednesday , 23rd Jan , 2019

Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kumtaka Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu Kurudi Tanzania, kigogo mwingine wa serikali amebainisha kuwa anamsubiri Mbunge huyo arejee nchini.

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu

Kauli hiyo imetangazwa na Mkurungenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geofrey Mwambe, ambapo amedai kuwa Tundu Lissu akirudi nchini atahakikisha lazima anakutana naye.

Kwa mujibu Mwambe amesema kuwa kitu pekee atakachohakikisha anamueleza kiongozi huyo ni kumjengea uelewa zaidi wa masuala ya uwekezaji badala ya kufanya upotoshaji wa mambo yanayofanywa na serikali ya Rais John Magufuli.

Lissu kwa sasa yuko kwenye matibabu nchini Ubelgiji baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi 30 mwishoni mwa mwaka 2017 alipokuwa Jijini Dodoma kwa ajili ya kutekeleza kazi zake za Kibunge.

Juzi, 21 Januari kupitia kwa Spika Ndugai, alimwambia Tundu Lissu kuwa hana kibali cha kukaa nje ya nchi badala yake anatakiwa kurudi Tanzania huku mwenyewe akibainisha kuwa atarudi kwa mujibu wa ripoti ya Daktari wake.