
Ubakaji
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo lilihudhuliwa na mama mzazi wa watoto hao aitwaye Lucia Hando ambapo baba yao aliwachukua watoto hao usiku wakati wamelala na kuwapeleka nyuma ya nyumba na kuwafanyia kitendo hicho huku akiwatishia kuwa angewachapa.
Katika tukio lingine, wananchi wa eneo la Mikumi Kwalaza, kata ya Mikumi mkoani Morogoro wamemkamata Askari wa Jeshi la Wananchi aliyejulikana kwa jina la Godlisten Remistone mwenye umri wa miaka 46 kwa kosa la kumbaka mwanafunzi.
Askari huyo wa kambi ya jeshi ya Suku wilayani Mikumi, alikamatwa na wananchi hao baada ya kukutwa akifanya mapenzi na mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mikumi.
"Baada ya kumkamata, alipelekwa kituo cha polisi cha Mikumi na anaendelea kushikiliwa mpaka sasa, uchunguzi unaendelea kufanyika kwaajili ya hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake", amesema Mutafungwa.