Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Akizungumza na Bw. Meng leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amesema kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni uendelezaji wa Makao Makuu Dodoma na hivyo serikali inatarajia mengi kutoka kwenye kampuni hiyo kutokana na China na Tanzania kuwa ni marafiki wa muda mrefu na mataifa hayo yanashirikiana vizuri katika ujenzi wa miundombinu.
“Dodoma kuna fursa za uwekezaji kwenye sekta nyingi kama miundombinu, kilimo na viwanda. Mnaweza kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba za makazi, ofisi, huduma za kijamii na viwanda ,”
Kwa upande wake Bw. Meng amesema kampuni yake itaungana na Serikali katika kuboresha Makao Makuu ya Serikali na inatarajia kutuma wataalam wake mkoani Dodoma kuangalia maeneo ya uwekezaji.
‘Nataraji tutakuwekeza katika ujenzi wa miundombinu, nyumba za makazi, ofisi, maeneo ya kutolea huduma za jamii na teknolojia zitakazowezesha upatikanaji wa maji safi na salama.