Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa vyama nchini Prof Ibrahim Lipumba, amesema wajumbe wa mkutano kuu wameridhia kumpatia majukumu hayo mapya bwana Khalifa.
Lipumba amesema "baada ya kupeleka majina mawili ya kupata Katibu Mkuu jina moja la Katibu Mkuu limerudi ambaye amechaguliwa ni Khalifa Suleiman Khalifa"
Aidha Magdalena Sakaya ametajwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho upande wa Tanzania bara.
Mpaka sasa upande wa Maalim Seif bado haujasema chochote juu ya maamuzi hayo.