Friday , 10th May , 2024

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamedi Mchengerwa ameapa kula sahani moja na viongozi wa sekta ya Afya wanaoshiriki kuzuia watumishi na watendaji kutopanda madaraja kwasababu zao binafsi.  

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Waziri Mchengerwa ametishia kuwaondoa kwenye nafasi zao viongozi wote wanaohusika kukwamisha watumishi kupanda madaraja katika ngazi mbalimbali huku akisisitiza jambo la watumishi kupandishwa madaraja kuwa ndio kipaumbele chake. 

Mchengerwa ameyasema hayo wakati akifungua maadhimisho ya 51 ya siku ya Wauguzi yanayofanyika Kitaifa Mkoani Tanga ambapo katika hotuba yake Rais wa chama cha wauguzi Tanzania Alexander Baluhya alisema jambo hilo limekuwa kilio chao cha muda mrefu sasa hususani kwa watumishi waliopo muda mrefu kazini. 

Kufuatia hatua hiyo Waziri Mchengerwa alimuagiza Mkurugenzi wa afya kusimamia jambo hilo kwa haraka ili kila mmoja mwenye sifa ya kupanda daraja apandishwe kulingana na anavyostahili.  

"Mkurugenzi wa afya nakukabidhi hili kama tumeweza katika maeneo mengine kwanini tushindwe kuwapandisha madaraja na kama kuna kiongozi yeyote anayekwamisha katika maeneo yenu anayezuia madaraja msipandishwe nitamuondoa kwenye nafasi yake, "alisisitiza

Katika hatua nyingine Waziri Mchengerwa ameameagiza kilaHalmashauri nchini kutenga fedha kwajili ya posho za watumishi pindi wanapoandaa mikutano kama hiyo kwakuwa mikutani hiyo ipo kisheria na kwenye bajeti kila mwaka. 

"Hata changamoto tulizonazo wakati mwingine ni kunyima haki tu haki zenu za msingi na ndio maana wakati mwingine mambo mengi ya hovyo hovyo yanatokea sasa hili sitakubali Mkurugenzi wa afya upo hapa peleka ujumbe huu kwa Katibu mkuu kwa kuwa sitakubali wale wote waliochini yangu sitaki nisikie hata kidogo kuna mtumishi anaonewa au ananyimwa haki zake za msingi kama za namna hii kwahiyo hili nitalisimamia, "alisisitiza waziri Mchsngerwa. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Tanga Balozi Dkt Batilda Burian amsema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu katika sekta ya afya walipata zaidi ya bilioni 67.9 fsdha zilizokwenda kufanya mambo makubwa ikiwemo ujenzi wa zahanati 72 huku bilioni 9 zikitumika katika ujenzi wa vituo vya afya 23.

Rais wa Chama cha wauguzi Tanzania Dkt Alexander Baluhya alisema kuwa kumekuwa na changamoto katika baadhi ya maeneo kwenye Halmashauri zao ikiwemo wauguzi kupangiwa majukumu yasiyo ya kwao yaliyopo nje ya taalumz yao hususani suala la kufanyishwa usafi. 

"Hili tumelifuatilia na tumeona ni miongoni mwa maeneo yanayoathiri utoaji wa huduma za afya mtu anajikita kutumia nguvu nyingi kwenye jambo ambalo si la kitaaluma na haliko kwenye wito wake mfano imeeleweka na kutafsirika kwamba wauguzi ni sehemu ya taaluma inayopaswa kufanya usafi lakini ukingalia miongozo yote haluna sehemu muunguzi anafundishwa kufanya usafi kwamaana ya kudeki lakini kuna baadhi ya maeneo wanawajibishwa kwasababu hawajafanya usafi katika maeneo hayo hili sio sawa,"alibainisha Rais wa wauguzi