
Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Kamanda Kitalika amesema amefanya ziara na helkopta kutathmini hali ya usalama, na kuona sehemu kubwa ya jiji ikiwa imejaa maji, hususan maeneo ya bonde la mpunga.
“Infact nimeruka kwa helkopta kutathimini general situation ya hapa, hali si nzuri, jiji lina hali mbaya sana nyumba nyingi zimezingirwa na maji hususan sehemu za Jangwani, sehemu ya bonde la mpunga, kwa ufupi maji ni mengi, sasa nilikuwa natoa wito kwa wale walioamua kuhama basi wasirudi haya maeneo haya, wale wa Jangwani wasifikirie kurudi”, amesema Kamanda Kitalika.
Sambamba na hilo Kamanda Kitalika amesema eneo la Temeke kumeripotiwa ajali moja ya nguzo kuangukia bajaji, lakini hakuna taarifa ya kifo na aliyekuwa kwenye bajaji alikimbizwa hospitali ya Temeke kwa matibabu kwa kuwa hakuumia sana.