
Akiongea wakati wa mkutano wa kubadilishana ujuzi na utafiti juu ya kilimo cha mseto cha ufugaji wa kuku, samaki na mbogamboga katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambacho kimeshirikisha vyuo mbalimbali ikiwemo Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Kitivo cha Kilimo (UDSM), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Kwame Nkuruma cha Ghana pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Denmark, Balozi Jensen amesema wanafunzi wafundishwe juu ya kilimo hicho.
Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Yohana Budeba amesema serikali inapanga mkakati dhabiti wa kutoa elimu kwa maofisa ugani wote nchini ili kuweza kuwaelimisha wakulima juu ya kilimo cha mseto hasa maeneo ya vijijini.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Saalam, Prof. Rwekaza Mukandala amesema kwa sasa kilimo hicho kinatija kutokana na mkulima kutumia eneo dogo kwa aajili ya kilimo cha aina tatu na kupata faida kubwa ambapo amesema maeneo yote yaliofanyiwa utafiti huo kumekuwa na faida kubwa.