Tuesday , 27th May , 2014

Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, sera, uratibu na bunge, William Lukuvi, amelazimika kutoa maelezo baada ya baadhi ya wabunge wa CCM na mbunge wa Chadema Tundu Lissu, kumtuhumu kuwa aliomba fedha kutoka kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii LAPF.

Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, sera, uratibu na bunge, mhe. William Lukuvi.

Akijibu tuhuma hizo Mhe. Lukuvi amekiri kuomba na kuwahi kupewa fedha na mfuko wa LAPF, fedha ambazo alizitumia katika shughuli mbalimbali za kuendeleza jimbo lake na kusema kuwa kufanya hivyo si kosa kama Mhe. Lissu anavyojaribu kuonyesha.

Kwa upande wake Mhe. Tundu Lissu alionekana kutoridhika na majibu ya Mhe. Lukuvi na kuendelea kusisitiza kuwa ni kosa kuchukua fedha kwenye taasisi na mashirika ambayo wabunge huwa ndio wanapaswa kuzisimamia.

Aidha, suala hilo pia lilimfanya Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka kusimama ili kulitolea ufafanuzi ambapo alisema mifuko hiyo huwa inatenga mafungu kwa shughuli mbalimbali za kusaidia jamii.