Friday , 13th Mar , 2015

Bidhaa zinazopimwa na kupata ithibati ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali nchini Tanzania, hivi sasa zitakuwa na fursa ya kupata soko zuri ndani na nje ya nchi kutokana na maabara hiyo kupata hati ya ubora wa kimataifa ya ISO.

Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele

Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele, amesema hayo leo wakati akitambulisha hati hiyo yenye namba za ISO 1900: 2008, iliyotolewa na mamlaka yenye jukumu la kutoa hati za ubora wa bidhaa yenye makao makuu yake jijini Paris nchini Ufaransa.

Kwa mujibu wa Profesa Manyele, kabla ya kupata hati hiyo bidhaa zilizokuwa zinapimwa na maabara hiyo zilikuwa zikipata ugumu wa kujitambulisha katika soko lakini baada ya kupata hati hiyo wafanyabiashara.

Katika hatua nyingine, serikali ya Tanzania imetiliana saini mkataba wa shilingi bilion 77 na serikali ya Japan kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kupita juu katika makutano ya eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam.

Akiongea wakati wa makubaliano hayo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacious Likwelile amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza mwezi Mei mwaka huu utasaidia kupunguza hali ya msongamano kwa wasafiri na usafirishaji wa mizigo.

Dkt. Likwelile ameongeza kuwa msaada huo wa fedha utasaidia kuondoa upungufu wa bajeti uliosababishwa na kushuka kwa thamani ya fedha pamoja na ongezeko la vifaa vya ujenzi na kuwa serikali ya Japani imekuwa ikithamini urafiki kati yake na Tanzania kwa zaidi ya miaka hamsini sasa.