Tuesday , 4th Jul , 2017

Waziri wa Katiba na Sheria  Palamagamba Kabudi amesema marekebisho ya  muswada wa sheria unakusudia kubadilisha vifungu vya sheria kwa kufuta baadhi ya vifungu  na kuviandika upya.

Hayo yamesemwa na Waziri Kabudi leo wakati akiwasilisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2017.

"Muswada huu unatokana na mapendekezo ya kamati zilizoundwa kuchunguza ubadhirifu na udanganyifu kwa baadhi ya makampuni yanayojihusisha na uchimbaji na biashara ya madini. Pia utafuta baadhi ya maneno kwenye vifungu vya sheria hizi, kuingiza maneno mapya na kuongeza vifungu vipya" Mhe.Prof. Kabudi".

Hata hivyo Prof. Kabudi ameongeza kwamba  Kamati zilibaini mapungufu  12 ambayo baadhi ni udhaifu makubwa katika usimamizi wa sheria ya madini, sheria ya madini ya mwaka 2010 kutotambua mamlaka ya umiliki wa maliasili za madini nchini, Kutokuwepo kwa masharti yanayoelezea bayana ushiriki wa serikali na watanzania kwenye sekta ya madini.