
Mbunge Jaguar
Jaguar anayekabiliwa na mashtaka ya uchochezi dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni, ameachiwa huru leo kwa dhamana ya Ksh 500,000 ambayo ni sawa na shillingi za Kitanzania milioni 11, laki mbili na elfu 7.
Akitoa uamuzi wake hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Francis Andayi alisema "Jaguar yuko na majukumu ya kuwalinda Wakenya na raia wote wa kigeni na iwapo atatoa matamshi ya aina hiyo tena, atachukuliwa hatua kali zaidi za kisheria"
Ikumbukwe kuwa Mbunge huyo alikamatwa kwa kutishia kuwafurusha wafanyabiashara wa nchi za kigeni kutoka Kenya akidai wamewapokonya Wakenya biashara zao.
Kesi dhidi ya Mbunge huyo wa Starehe inategemewa kusikilizwa tena Julai 17 mwaka huu.