
Jopo la Majaji nchini Nigeria
Chama cha wanasheria na makundi ya haki za binadamu wamelaani hatua hiyo wakisema ina lengo la kukabiliana na wapinzani wa kisiasa.
Msemaji wa Rais Muhammadu Buhari amesema operesheni hiyo ni sehemu ya jitihada za kukabiliana na rushwa na si kwa ajili ya kuishambulia mahakama.
Polisi wa upelelezi wamefanikiwa kuzikamata dola laki nane na kuwaweka kizuizini majaji saba wanaotuhumiwa kwa rushwa.
Buhari, kiongozi wa zamani wa kijeshi alichaguliwa mwaka uliopita baada ya kutoa ahadi ya kukabiliana na tatizo sugu la rushwa na kuokoa fedha za umma zilizoibwa.