Thursday , 24th Jan , 2019

Baraza la Mitihani la Taifa NECTA limebainisha kufuta matokeo ya wanafunzi wawili ambao waliandika matusi kwenye mitihani yao kitaifa ya kidato cha nne ambao walifanya mtihani wao Novemba 2018.

Wanafunzi

Uamuzi huo umebainishwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dkt Charles Msonde Jijini Dodoma ambapo alitangaza kuwafutia matokeo takribani watahiniwa 252 kutokana na udanganyifu.

Akizungumzia tukio hilo Msonde amesema kati ya watahiniwa hao waliofutiwa matokeo, watahiniwa 71 walikuwa ni wa kujitegemea ambapo wawili walifutiwa kwa makosa ya kuandika matusi kwenye mtihani huo.

Aidha Katibu huyo amesema kuwa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limemtangaza kijana, Hope Mwaibanje kuwa ni mtahiniwa bora kitaifa kwa waliofanya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne Novemba mwaka jana. Shule ya Mtakatifu Francis ya Mbeya imekuwa ya kwanza kitaifa.