Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii Bw. Ephraim Kwesigabo
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii Bw. Ephraim Kwesigabo amesema hayo leo wakati akitoa taarifa ya mfumuko wa bei na kwamba kushuka huko haimaanishi kwamba bei ya huduma na bidhaa nchini imeshuka.
Kuhusu uwezo wa shilingi katika manunuzi, Bw. Kwesigabo amesema shilingi mia moja ya Tanzania inaweza kufanya manunuzi yenye thamani ya shilingi 97 na senti 04 huku mfumuko huo wa bei ukiwa haujatofautiana sana na ule wa nchi jirani za Kenya na Uganda.