
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye ameyasema hayo leo wakati akitoa maoni ya sekta binafsi kwenye mkutano wa majadiliano kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na China hususani katika eneo la biashara na uwekezaji.
"Ili kukuza ushirikiano uliokuwepo hapo awali namuomba DKt. John Mgufuli aweze kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na Rais mwenzake wa China kwani yeye ana ushawishi mkubwa wa wapi wawekezaji wake wanapaswa kwenda kuwekeza" Dkt Simbeye.
Akijibu hoja ya Simbeye, Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango amesema ushirikiano wa biashara kati ya Tanzania na China bado ni mzuri na kwamba kinachotakiwa ni kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa za kibiashara zinazopatikana katika taifa hilo.