Wednesday , 30th Apr , 2014

Mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), uliokuwa umezuiwa kupisha sherehe za Muungano utafanyika leo katika viwanja vya Kibandamaiti, Unguja baada ya kupata ruhusa ya polisi.

viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA. Kutoka kushoto ni Freeman Mbowe wa Chadema, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF na James Mbatia wa NCCR Mageuzi

Mkutano huo ambao awali ulikuwa ufanyike Apili 19, ulizuiwa na polisi kwa madai kuwa intelijensia yao iliyonyesha kuwa kungekuwa na tuishio la maisha ya watu, hivyowalishauriwa wapange tarehe nyingine baada ya sikukuu ya pasaka.

Msemaji wa polisi Zanzibar Mohammed Mhina alithibitisha kuruhusiwa kwa mkutano huo na kuwataka wananchi watakaohudhuria kuwa watulivu kabla na baada ya mkutano. Mkutano huo unatarajiwa kuanza saa 8 Mchana.