
Msemaji wa taasisi ya tiba za mifupa na mishipa ya fahamu Muhimbili - MOI (aliyekaa katikati), Almas Jumaa, akizungumza na waandishi wa habari Idara ya Habari Maelezo hivi karibuni.
Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) imesema idadi ya wagonjwa wanaopokelewa kutokana na ajali za barabarani zinazotokana na piki piki maarufu kama bodaboda pamoja na Bajaj zinazidi kuongezeka kwa kasi ambapo kwa wastani kwa siku wanapokea wagonjwa kati ya watano hadi 20.
Hayo yameelezwa leo Jiji Dar-es-Salaam na Afisa Uhisiano wa MOI Bw. Almasi Jumaa wakati akielezea ujenzi wa jengo jipya la taasisi hiyo ambalo limegharimu takribani fedha za Tanzania shilingi bilioni 30.
Amesema ujenzi wa jengo hilo la kisasa litasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaopelekwa katika taasisi hiyo kutokana na sasa kuwa na msongamano mkubwa wa wagonjwa unaoepelekea wagonjwa wengine kukosa sehemu za kulala.