Tuesday , 8th Nov , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amelionya jeshi la polisi mkoani humo pamoja na maafisa ustawi wa jamii, kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia lengo likiwa ni kupunguza vitendo hivyo katika jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

 

Mkuu wa Mkoa huyo ametoa onyo hilo mkoani Mwanza wakati akizindua kituo jumuishi cha huduma kwa waathirika wa ukatali wa kijinsi na kusema kuwa lazima vitendo hivyo vikomeshwe mkoani humo.

Mongella ametoa takwimu za ukatili wa kijinsia mkoani humo na kusema kuwa mkoa huo ni kati ya mikoa inayoongoza kwa ukatili wa kijinsia kutokana na kubainika kuwa mkoa una asilimia 51 ya matukio ya ukatili huo kwa watu tofauti ikiwemo watoto na wanawake.

Mhe. Mongela amesema kuwa kuna baadhi ya askari polisi wameripotiwa kuwa chanzo cha kikwazo cha kupatikana kwa haki kwa watu wanaofanyiwa vitendo vya kijinsia hivyo suala hilo linapaswa kutatuliwa haraka iwezekanavyo.