Thursday , 21st Dec , 2017

Naibu wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Damian Green, amefukuzwa kazi baada ya kubainika kuwa alikiuka kanuni za uwaziri kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu picha za ngono zilizokutwa kwenye kompyuta yake.

Bwana Green ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa Waziri mkuu Theresa May alibainika kuwa alitoa taarifa zisizo sahihi kuhusu picha za ngono zilizokutwa kwenye komputa yake ya ofisini.

Aidha Bw. Green alikuwa anachunguzwa pia juu ya madai ya kutowaheshimu wanawake wanaharakati katika chama chake cha Conservative.

Hata hivyo kiongozi huyo amekanusha kuhusika na mashitaka yote yanaomkabili.