Thursday , 19th May , 2016

Ndege ya Shirika la Ndege la Misri iliyokuwa ikitokea Jijini Paris nchini Ufaransa kuja Cairo Misri imetoweka kwenye rada, taarifa za shirika hilo zimesema.

Taarifa hiyo imesema ndege hiyo MS804 ilikuwa na abiria 56 na watumishi 10, wakati ikitoweka.

Ndege hiyo ilikuwa angani umbali wa futi 37,000, wakati ilipotoweka mashariki mwa Mediterranean.

Shirika la ndege la Misri limesema litatoa taarifa zaidi litakapopata taarifa mpya kuhusu tukio hilo.