Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

NEC yafanya uteuzi, CCM yaramba dume

Saturday , 21st Jul , 2018

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeteua madiwani nane wa Viti maalum wa CCM na CHADEMA kujaza nafasi zilizoachwa wazi katika halmashauri nane za Tanzania bara, ambapo CCM yenyewe imefanikiwa kupata nafasi tano huku tatu zikienda CHADEMA.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage.

Hayo yamewekwa wazi na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage leo Julai 21, 2018 na kusema uteuzi huo umefanyika baada kukaa kikao cha tume hiyo cha Julai 19, 2018.

Walioteuliwa ni Ajila Kalinga (CCM-Songea), Mary Kazindogo Mbilinyi (CCM Makete), Zainab Abdu Mabrouk (CCM-Kongwa), Restuta Aloyce Gardian (CCM-Muleba), Siglinda Silvester Ngwega (CCM-Morogoro).

Wengine ni Zena Said Luzwilo (CCM-mji Kahama), Neema Michael Massawe (Chadema Monduli) na Teodola Muyula Kalungwana (Chadema-Iringa).

"Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya Serikali za mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa aliitarifu tume ya uchaguzi kuwepo kwa nafasi hizo wazi za madiwani wanawake wa viti maalum kupitia CCM na CHADEMA", amesema Jaji Kaijage.

Uteuzi huo wa madiwani wa CHADEMA na CCM umekuaja baada ya walioteuliwa awali kufariki dunia pamoja na wengine kujiuzulu.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi