
Akizungumza Mjini Bagamoyo Mama Salma Kiwete amesema kuna mikoa ambayo haina Ng'ombe wa kutosha kuweza kupata kinyesi cha kutengenezea Nishati hiyo ila amewataka wataalamu kufikiria nja mbadala na kufanya utafiti wa ziada ili kuweza kusambaza nishati hiyo.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi amesema kuwa lengo la serikali kusisitiza mradi huo ni kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ili kulinda mazingira lakini pia ni kufikisha umeme vijijini kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi
Waziri wa uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe ametoa onyo kwa Wafanyakazi wa shirika la Reli nchini Tanzania TRL kwa kusema kuwa atawawajibisha wale wote watakaobainika kulihujumu shirika hilo.
Dk. Mwakyembe amesema hayo wakati akiongea na Madereva wa Treni mjini Dodoma katika kiako cha kuboresha shirika hilo na kusema TRL inasifa ambayo sio nzuri kwa wateja wake na kuongeza kuwa pindipo atakapoabaina yoyote anelihujumu shirika hilo hatosita kumchukulia hatua kali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la reli Nchini Mhandisi Kipako Kisavu amesema katika kuboresha shirika hilo na kuondoa msongamano wa mizigo bandarini shirika hilo limeingia mkataba na mamlaka ya Bandari nchini ili kusaidia kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi.